Mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wa kujulikana kwa neno ‘‘Waashi Huru’’ au kwa kingereza ‘Freemasons’ nchini Tanzania. Neno hili lilikuwa kinywani kwa kila mtu mjini na vijijini ikisaidiwa na magazeti ya udaku ambayo mengi huandika habari zao bila utafiti wowote.

Kutokana na maelezo ya Wikipedia inaonyesha kuwa Freemasons ni wajenzi/waashi  huru na hujitungia sheria na kanuni zao za kazi na mikutano. Mfano moja ya kanuni yao ni kutofanya kazi usiku na  usichukue kazi ambayo hutaweza kuifanya n.k. Kwa ujumla, sheria hizi ni nzuri kwa mtu yoyote yule bila hata kuwa ni mwanachama wa Freemasons au lah.

Bahati mbaya kwa watanzania wengi walidhani wanajua Freemasons ni nini kumbe wasijue ukweli wenyewe. Wengi wao waliodhani wanajua kuhusu ‘Waaashu Huru’ walikuwa ni waongo na wapotoshaji na wanaochukulia mambo kijujuuu. Ni watu wenye mawazo mepesi ndio maana walihusisha freemasons na vitu vya hovyo hovyo bila kujua ukweli.

Kwa mfano, mapema mwaka 2012 Twaweza/Uwazi walizambaza simu za mikononi kwa baadhi wa wakazi wa maeneo mbalimbali Tanzania kama sehemu ya utafiti wa ‘Sauti Za Wananchi’ kusikia sauti za wananchi juu ya huduma za kijamii na mambo mengineyo. Baadhi ya wakazi walichaguliwa kwa njia ya bahati nasibu kushiriki zoezi hilo kwa njia ya simu ambapo Twaweza/Uwazi huwapigia simu baada ya kipindi fulani na kuwauliza maswali husika. Teknologia ya simu imerahisisha maisha sana, asante kwa teknologia.

Kilichotokea kwa baadhi ya wakazi waliokosa simu zile kwa bahati nasibu kushiriki zoezi wakazusha kuwa simu walizopewa jirani zao, wanakijiji, wanajamii wenzao zinatokana na Freemasons na kwamba baadhi ya watu waliopewa na kutumia simu hizi watatu wameshafariki mjini Morogoro!!! Kitu ambacho haikukwa na uweli wowote.

Habari mbaya husambaa mapema na kwa haraka, mara kila mkoa ulioshirikishwa katika zoezi la ukusanyaji wa taarifa kwa njia ya simu kukawa na wakala wa kusambaza taarifa kuwa simu za Twaweza/Uwazi zinatokana na Freemasons. Lakini, nini kilisababisha haya?

Mwezi Desemba, 2012, rafiki yangu Hozee alienda duka la kubadilisha pesa za kigeni Posta akiwa $ 500 ili kubadili kuwa za shilling. Kama kawaida ya baadhi wa wafanyakazi wasiopenda kazi zao au kuwa na ukarimu kwa wateja, dada wa duka la fedha alikuwa na kiburi kwani baada ya kubadilisha pesa ile akatupa pesa hovyo mezani bila mpangilio. Hozee akamwomba azikusanye zile pesa vizuri ikiwezekana azifunge na lastiki. Dada yule akazikusanya bila lastiki na kumpatia Hozee, Hozee akamwomba tena aziweke katika bahasha kwa kuwa kwenye mfuko zingetuna sana.

Mhudumu yule kwa kukosa nidhamu ya kazi na huduma kwa wateja akaghahirisha huduma ya kubadilisha fedha na kumwita Hozee Freemason na kumshutumu kuwa hakuwa pale dukani kwa huduma ya kubadilisha fedha bali kitu kingine ambacho mhudumu alidhani ni ‘Ufreemason’.

Tafakari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *